“Kuwapa watoto sumu” – nyakati za wamishenari
Mwaka 2003, nilijitolea kumsaidia mmishenari aliyekuwa akifanya kazi na watoto, na hapo ndipo shauku ya kuwafikia watoto ilikua ndani yangu. Mimi na mke wangu, Nancy, tulifanya kazi na mmishenari kutoka tamaduni nyingine hadi alipotuachia jukumu la kuendelea na kazi hiyo na yeye akarudi kwao.Tulipoendelea kuwafikia watoto, tulitambua hitaji kubwa la huduma kwa watoto katika eneo la kusini mwa Afrika. Mwaka 2014 tukawa wamishenari wa kudumu. Kwa bahati mbaya, haikuonekana kama kulikuwa na mazingira wezeshi kwa ajili ya huduma ya kuwafikia watoto. Tuliandaa mtaala maalum kwa ajili ya kuwafikia watoto – mfululizo wa vitabu sita vinavyoitwa Today for Tomorrow (Leo Kwaajili ya Kesho). Vitabu vitatu vya kwanza vilianzishwa tukiwa pamoja na yule mmishenari mwenzetu, na sisi tukakamilisha vitabu vitatu vya mwisho. Mwongozo huu sasa umetafsiriwa kutoka Kiingereza hadi lugha takriban nane tofauti.
Ili kuwafikia watoto wapya, tunaanza na “mkono wa injili.” Tunatumia kila kidole kuelezea hitaji la wokovu na jinsi tunavyopata wokovu kwa kumwamini Yesu. Tunatembelea shule moja kila wiki hadi tuone kuwa watoto wameelewa. Kupitia njia hii, watoto wengi wamekuja kumwamini Yesu.
Kazi ni kubwa na nzito; tunafanya kazi na watu wengi wa kujitolea. Wakati mmoja tulimshirikisha mfanyakazi wa huduma ya watoto vifaa vyetu, akasema, “Nimekuwa nikiwapa watoto sumu kwa sababu sikujua nini cha kuwafundisha.”
Kuwaona watoto wakimpokea Kristo kama Mwokozi wao kunaufurahisha moyo wangu sana. Hilo ndilo lengo letu kuu kabisa.
Soma hadithi yote kwa Kiingereza hapa https://afrigo.org/…/missionary-profile-chris-and…/