Skip to content

“Ndoto yangu niliyosubiri kwa muda mrefu” – nyakati za wamishenari

Kirubel Girma, mhamasishaji wa misheni wa Ofisi ya Kutuma Wamishenari ya SIM Ukanda wa Afrika Mashariki iliyoko Addis Ababa, Ethiopia, anasema: “Hatimaye nimeanza kutimiza ndoto yangu ya muda mrefu ya kuhudumu kama mmishenari wa wakati wote, nikiwa na lengo la kuhamasisha, kuwezesha na kuwatuma wamishenari kutoka Afrika Mashariki kwenda katika kazi ya misheni kimataifa”
Licha ya changamoto zilizosababishwa na janga la COVID-19, Kirubel anashangazwa na dhamira thabiti na shauku isiyotetereka ya makanisa ya hapa ya wenyeji na watu wenye matarajio ya kazi ya misheni. Anaongeza: “Tumekuwa tukifanya kazi ya kuwatuma wanandoa wanane na watu watano wasiooa/olewa kutoka Ethiopia, Kenya, Eritrea, Rwanda, Uganda na Tanzania. Lengo letu kuu ni kuwafikia jamii ambazo hazijafikiwa kabisa na injili.”
Lengo lake la kwanza la miaka mitano ni kuona angalau kanisa moja kutoka katika kila moja ya nchi 11 za Afrika Mashariki likiwa limehamasishwa kwa ajili ya misheni.
“Nimejawa na furaha kwa kuwa Mungu amenipitisha katika safari hii hadi sasa naweza kusaidia wamishenari kutimiza kwa mafanikio misheni zao katika maeneo mbalimbali.”
Tafadhali MUOMBEE Kirubel anapohudumu kama mhamasishaji wa misheni Afrika Mashariki.
Soma hadithi yote kwa Kiingereza kupitia https://afrigo.org/stor…/missionary-profile-kirubel-girma/
share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us