Skip to content

“Hatukuwa na pesa” – nyakati za wamishenari

Wakati nilipokuwa kwenye masomo ya kuwa mchungaji katika Chuo cha Biblia cha Kiinjilisti cha Malawi (EBCoM), nilikuwa na wanafunzi wenzangu wengi kutoka Msumbiji. Walikuwa wakiniambia mara kwa mara, “Kuna wachungaji wengi Malawi, lakini Msumbiji wapo wachache sana, ilhali tuna makundi mengi ambayo bado hayajafikiwa. Kwa hiyo kwa nini usije ukafanya kazi pamoja nasi Msumbiji?”
Nilifikiria na kuomba kuhusu jambo hilo kwa muda mrefu, na kadri walivyoendelea kunisihi, shauku yangu ilikua. Lakini nilipomaliza masomo ya Biblia na kuwaeleza viongozi wangu maono yangu, ilibainika kuwa siwezi kwenda.
Nilifanya kazi kama mchungaji, lakini wito wa kuwa mmishenari uliendelea kunikaa moyoni mwangu kwa miaka tisa. Siku moja, nilikutana na mhamasishaji wa misheni aitwaye Watson Rajaratnam. Aliniuliza kuhusu wito na maono yangu. Nikamweleza hamu yangu ya kuwafikia wasiofikiwa nchini Msumbiji. Aliwaendea viongozi wangu na kuzungumza nao. Pia alizungumza na shirika la kimisheni, SIM.
Nilikuwa na tatizo moja – hatukuwa na pesa. Kisha siku moja, mwanaume aliyekuwa akistaafu kazi yake alitupatia milioni moja ya Kwacha ya Malawi. Tulijua kabisa kuwa ni Bwana aliyetoa huo msaada! Mwaka 2018, mimi na mke wangu Elina hatimaye tulikwenda Msumbiji kama wamishenari.
share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us