fbpx Skip to content

Kwa wakati kama huu

By Sam Ngugi

Sote tunahusika kwa namna fulani katika ‘sanaa’ ya uhamasishaji, kutia moyo na kushawishi wengine katika mwelekeo fulani. Kutokana na mtazamo huu, kila mtu ni mhamasishaji, lakini ikiwa ni Agizo Kuu, basi huwa ni muhimu sana.

Hata hivyo, huduma ya uhamasishaji ina mwelekeo mwingine muhimu na tofauti; inabeba ufahamu na ubora wa wito wa mtu binafsi. Mhamasishaji ana msukumo wa kiroho wa ndani, wajibu na shauku ya kutia moyo, kutia changamoto na kuwaita watu wa Mungu wajihusishe na ajenda ya ufalme wa Mungu. Wahamasishaji ni wenye kuleta mageuzi, wakiwaonyesha watu kutoka ‘hali ilivyo’ hadi ‘inavyopaswa kuwa’ na kuwapa watu wa Mungu maono kwa ajili ya viwango vya juu na ajenda pana ya ufalme. Wanawatia watu msukumo wa ujasiri, kuwa na imani, na kuwa tayari kujitoa mhanga. Mhamasishaji hupata ufahamu wa kusudi la maisha yao pale wanapoona watu wa Mungu wakitoa maisha yao yote kwa Mungu na kwa kusudi lake la milele. Wahamasishaji husafiri katika mahusiano na huishi katika kutafuta kusudi la utukufu wa Mungu miongoni mwa mataifa.

Tunaishi katika kipindi nyeti katika historia ya kanisa ambapo ukristo unapitia ukuaji wa ajabu katika sehemu ya Kusini mwa dunia, ilhali unapungua kwa kasi katika mataifa ya magharibi. Wakati huo huo, utandawazi, uhamaji na misukosuko mingi ya dunia inatoa fursa za kipekee kwa kizazi hiki na hivyo kurahisisha mwingiliano wa tamaduni katika kufanya umisheni, ushirikiano wa kimkakati, na matazamio ya mavuno makubwa katika historia ya kanisa.

Kwa kweli, Mungu anaanzisha huduma ya umahamasishaji wakati huu, akiwaita wahamasishaji kutoka kote ulimwenguni kuungana na kanisa lake kwa ajili ya mavuno ya ulimwengu.

Kutoka upande wa kusini wa dunia hadi upande wa kaskazini, kutoka kwenye miji kwenda vijijini, vijana kwa wazee, wanaume kwa wanawake, wanatheolojia kwa walei, wahandisi kwa wajasiriamaliwahamasishaji wanapiga tarumbeta wakiita watu wote wa Mungu kujihusisha kikamilifu na Agizo Kuu. Wahamasishaji wa muda wote, wakiwa wamejitoa kwa kazi ya uhamasishaji kwa muda wao wote katika nguvu za Roho Mtakatifu, watakuwa wenye kuleta mabadilikoa kwa kazi ya umisheni duniani katika wakati wetu. Uhamasishaji wa bidii, usio na ukomo, na wa kimkakati ungeweza kuachilia nguvu kubwa ya umisheni unaohusisha jamii zote duniani kwa namna ambayo haikuwahi kuonekana. Tunaona mguso wa aina hii katika Afrika.

Katika toleo hili la AfriTwende, utasoma habari za kusisimua za wanaume na wanawake wanaohamasisha makanisa kuamka kwa ajili ya kazi ya Umisheni katika mataifa. Utafurahia kusoma makala ya Kaka Kehinde Ojo ambaye, pamoja na mafanikio yote kwa viwango vya ulimwengu huu, aliamua kuitikia wito wa kazi bora zaidi kutoka juu! Tony na Julia, wanandoa vijana na wenye nguvu ambao nimewafahamu kwa miaka kumi, wanashirikisha ushuhuda wao wa kushangaza kama wahamasishaji wa muda wote, waliojitoa katika kuelimisha makanisa katika nchi ya Kenya kuhusika katika kazi ya umisheni duniani. Timu ya AfriTwende inachukua kurasa mbili kushirikisha rasilimali za uhamasishaji kama vile kutoa kozi za masomo ya Biblia kwa njia ya mtandao, na mengine mengi. Pia tunatoa taarifa juu ya vijana watano ambao walitumika katika safari fupi za umisheni na jinsi safari hizo zinavyoweza kuhamasisha watu binafsi na makanisa yanayowatuma.

Nafsi zenu na zihuishwe na kila mhamasishaji athibitike na kufarijika katika shughuli ya kupiga tarumbeta kwa ajili ya kazi ya Mungu ya umisheni katika bara lote la Afrika.

“Uhamasishaji ni mchakato wa kuwatia maono na kuwaelimisha watu wa Mungu kuhusu mipango yake kimkakati kwa ajili ya ulimwengu. Ni njia ya kuwahifadhi wale wanaohusika na wanaoendelea mbele mpaka wapate mahali na nafasi yao ya pekee katika ulimwengu wa uinjilisti.” – Na Fred Markert, GlobalCAST Resources

4.4 Sam Ngugi

Sam Ngugi na mkewe Harriet ni waasisi na viongozi wa Ushiriki wa Kampeni ya Umisheni (Mission Campaign Network), ambao ni shirika la uhamasishaji likifanya kazi kuendeleza dhima na maono miongoni mwa wanafunzi wa vyuo na makanisa katika Afrika Mashariki. Pia walizindua GEN 12 – Shirika la Umisheni kwa ajili ya kutuma wamishonari wa kiafrika katika makundi ya watu ambao kwa kiasi kikubwa bado hawajafikiwa. 

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us